Na Leonard Murunga
Mwenyekiti wa timu ya Muhoroni Youth FC Moses Adagala, ameapa kuhakikisha kuwa timu hiyo inarejea kwenye ligi kuu ya soka nchini – FKF PL haraka iwezekanavyo, akionya kuwa 'chuma cha wapinzani wao ki motoni.'
Muhoroni Youth FC na Nzoia Sugar zilishushwa daraja mwishoni mwa msimu jana, na sasa zinajiandaa kuonyeshana ubabe kwenye ligi ya daraja la pili, yaani NSL msimu huu.