Na Jabali Media
Huenda klabu ya Nzoia Sugar FC imefika mwisho wa reli.
Hii ni baada ya usimamizi wa kampuni ya sukari ya Nzoia kupitia mwenyekiti wa bodi, aliyekuwa mbunge wa Kanduyi Alfred Khanga'ti, kusema kuwa hawana misuli ya kifedha kuendelea kuifadhili timu hiyo.
Nzoia Sugar FC ilishushwa ngazi kutoka ligi kuu ya soka nchini (FKFPL), hadi ligi ya daraja la pili (National Super League), mwishoni mwa msimu jana.
Kwenye NSL msimu huu, vijana hao ambao huandaa mechi za nyumbani ugani Sudi mjini Bungoma, wameshiriki mechi nne ila hawajapata ushindi. Matokeo ni kama ifuatavyo:
Nzoia Sugar FC 1-1 Fortune Sacco
Nairobi United 0-0 Nzoia Sugar FC
Nzoia Sugar FC 0-1 APS Bomet
Darajani Gogo 3-1 Nzoia Sugar FC
Ratiba ya mechi za Nzoia Sugar FC hadi Desemba 15 ni kama ifuatavyo:
Nzoia Sugar vs Migori Youth (wikendi hii)
Mombasa United vs Nzoia Sugar FC
Dimba Patriots vs Nzoiia Sugar FC
Nzoia Sugar FC vs Mofa AC
Sam West FC vs Nzoia Sugar FC
Nzoia Sugar FC vs Naivas FC
Nzoia Sugar FC vs Vihiga United
Kibra United vs Nzoia Sugar FC
Nzoia Sugar FC vs Kisumu All Stars
Timu hiyo, licha ya kunoa vipaji vya baadhi ya wachezaji tajika humu nchini awali, inakabiliwa na hatari ya kufutika katika ubao wa kandanda ya Kenya.
Taarifa na picha kwa hisani ya mwanahabari Duncan Kwobah.
Mwisho wa reli kwa Nzoia Sugar FC?
Tools
Typography
- Smaller Small Medium Big Bigger
- Default Helvetica Segoe Georgia Times
- Reading Mode