Na Jabali Media
Baadhi ya wakazi wa Kisumu wameapa kumpigia kura rais William Ruto, ikiwa atatimiza ahadi zake kwao kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Rais Ruto alikuwa Kisumu mnamo Jumanne kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili.
Alifungua rasmi kongamano la nne la AfSNET, kabla ya kuwahutubia wana Kisumu katika maeneo ya Kondele na Kisumu mjini.
Sawa na safari yake ya Kisumu mwezi Agosti, Ruto alitoa ahadi kem kem, ikiwemo kuekeza kima cha shilingi bilioni 2.7 kufanikisha ujenzi wa kituo cha kudhibiti visa vya ajali Ziwani Victoria.
"Tunawekeza shilingi bilioni 2.7 ili kushughulikia changamoto ya ajali Ziwani Victoria haraka iwezekanavyo,” akasema rais.
Wakizungumza siku moja baada ya Ruto kuzuru Kisumu, baadhi ya wakazi wakiongozwa na Obungu Owich, Ambrose Otieno na Beatrice Amondi wamempongeza kwa mipango yake kwa wakazi wa Nyanza.
Owich amemtaka kiongozi wa nchi kurejesha mpango wa Kazi Mtaani, ili vijana wasio na ajira wapate ajira, akiongeza kuwa visa vya uhalifu jijini Kisumu vinachochewa na ukosefu wa kazi miongoni mwa vijana.
“Rais alikuja na ahadi nyingi na tumaini letu ni kwamba atazitimiza. Akizitimiza, sisi wakazi wa Kisumu hatutakuwa na lingine ila kumpigia kura kwa wingi mwaka 2027,” akaongeza Ambrose.
Naye Beatrice amempongeza rais kwa mpango wa kujenga kituo cha samaki kutua jijini Kisumu, akisema kuwa kitakuwa cha kipekee miongoni mwa kaunti tano zinazopokana na Ziwa Victoria.
Timiza ahadi tukupigie kura 2027, wakazi wa Kisumu wamrai rais Ruto
Typography
- Smaller Small Medium Big Bigger
- Default Helvetica Segoe Georgia Times
- Reading Mode