Tieni bidii shuleni, wanafunzi waambiwa

News
Tools
Typography
  • Smaller Small Medium Big Bigger
  • Default Helvetica Segoe Georgia Times

Na Leonard Murunga

Wanafunzi waliopata uja uzito na kupewa fursa ya kuendeleza masomo yao baada ya kujifungua katika kauti ya Kakamega, wamehimizwa kutia bidii kwenye masomo yao ili waweze kujikimu maishani siku za usoni.

Akizungumza katika hafla iliyowaleta pamoja wanafunzi ambao wanafadhiliwa na wakfu wake wa Janet Barasa, Bi. Barasa ambaye ni mke wa gavana wa Kakamega Fernandes Barasa, amewahimiza wazazi hao wachanga kuwa kielelezo katika jamii.

“Mna wajibu wa kutia bidii masomoni, alisema Bi. Barasa.

Kauli yake iliungwa mkono na Afisa Mkuu wa Elimu, Sayansi na Teknologia katika kaunti ya Kakamega Vivian Ayuma.

Ayuma ameitaka serikali kudhibiti matumizi ya mitandao ambayo mara nyingi inachangia watoto kuingia katika mitego mbali mbali, huku akihimiza viongozi wa kidini, walimu, wazazi pamoja na jamii kwa ujumla kuwa kwenye mstari wa mbele kuwaongoza kimaadili watoto.

Kwa upande wao, Dorothy Okemo na Mary Makokha wanaoshirikiana na wakfu wa Janet Barasa, wamesema kuwa ushirikiano huo ni wa kusaidia jamii ili kupunguza na kuzuia visa vya mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi wa kike.

Wameitaka serikali kuwakabili ipasavyo, washukiwa wa visa vya dhuluma za kijinsia katika jamii.