Yego Mobility yazindua huduma za teksi jijini Kisumu

Yego Mobility yazindua huduma za teksi jijini Kisumu. Picha/OO

News
Tools
Typography
  • Smaller Small Medium Big Bigger
  • Default Helvetica Segoe Georgia Times

By Jabali Media

Kampuni ya Yego Mobility, imezindua huduma za teksi jijini Kisumu.

Uzinduzi huo unaashiria mikakati ya upanuzi ambayo imekuwa ikiendeshwa na kampuni hiyo ya kutoa huduma za teksi kidigitali.

Kwenye kikao na makumi ya madereva wa teksi wakati wa uzinduzi huo kwenye hoteli moja jijini Kisumu hii leo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Yego Mobility Karanvir Singh, amesema kwamba lengo lao ni kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kupitia madereva.

“Tuko hapa kwa sababu yenu. Bila nyinyi, sisi hatupo,” akasema Singh.

Ameongeza kwamba wameweka mikakati kabambe ya kuwawezesha kifedha madereva wa teksi, ikilinganishwa na washindani wao katika soko la huduma za teksi kidigitali.

“Tunaamini katika kuwawezesha madereva kabla ya kuwazia faida. Tuko wazi, tunaendesha shughuli zetu kwa kuzingatia sheria na kwa njia ya uwajibikaji,” akaongeza afisa huyo mkuu mtendaji.

Naye Imran Omoth, mwenyekiti wa Kisumu Digital Cabs Association (KDCA) amesema kwamba kati ya madereva 300 na 400 tayari wamejiunga na kampuni hiyo, baada ya kuahidiwa matokeo bora kifedha.

“Suala la mapato limekuwa nyeti katika biashara hii kwa mda mrefu. Chini ya Yego, tunatarajia kupata asilimia 82 ya mapato,” alisema mwenyekiti huyo.

“Tunatarajia kwamba Yego itakuwa bora,” akaongeza Paul Omolo, Katibu Mkuu wa KDCA.

Bima ya afya na malipo bora ni miongoni mwa manufaa watakayopata madereva, huku abiria nao wakiahidiwa usalama wa kutosha wakati wa safari, kama mojawepo ya huduma za Yego Mobility.  

Yego Mobility tayari inaendesha shughuli za teksi katika kaunti za Nairobi, Nakuru, Eldoret, Mombasa na maeneo mengine ya ukanda wa Pwani.

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.