15
Tue, Oct

TSC yatangaza nafasi 46, 000 za ajira

Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC Nancy Macharia. Picha/Hisani

News
Tools
Typography
  • Smaller Small Medium Big Bigger
  • Default Helvetica Segoe Georgia Times

Na Jabali Media

Tume ya Huduma Kwa Walimu nchini (TSC), imetangaza nafasi 46, 000 za ajira.

TSC inalenga kuwaajiri walimu 6,000 kwenye shule za msingi, 39,550 kwenye shule za sekondari msingi (JSS) na 450 kwenye shule za upili kote nchini.

Wanaolenga nafasi hizo wamehimizwa kutuma maombi kupitia tovuti ya tsc.go.ke au teachersonline.tsc.go.ke kufikia tarehe 7 mwezi huu.

Wanao-omba nafasi ya ualimu kwenye shule za msingi wanafaa kuwa na cheti cha P1, huku wale wa JSS na shule za upili wakitakiwa kuwa na angalau cheti cha diploma.

Wanaohudumu chini ya mpango wa kujipatia tajriba yaani internship, pia wamehimizwa kutuma maombi yao, huku wakihitajika kuwasilisha vitambulisho vyao vya taifa, wakati wa zoezi la kudhibitisha uhalali wa vyeti vyao.

Tangazo hilo la TSC linajiri mwezi mmoja baada ya wakuu wa Chama cha Kutetea maslahi ya walimu wa shule za sekondari na Vyuo vya Kadri (KUPPET), kusitisha mgomo uliodumu wiki moja pekee.

Wakuu wa KUPPET waliitisha mgomo huo, ili kushinikiza utekelezaji wa makubalino ya pamoja (CBA) ya mwaka 2021-2025, pamoja na kuajiriwa kwa walimu wa JSS miongoni mwa matakwa mengine.

“Tunasitisha mgomo na kuwaagiza walimu wote kurejea kazini tukisubiri utekelezaji wa haraka wa masuala mbali mbali jinsi tulivyokubaliana na wakuu wa TSC,” alisema Katibu Mkuu wa KUPPET Akelo Misori, tarehe mbili mwezi Septemba.

Kauli yake ilitiliwa mkazo na Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa TSC Nancy Macharia.

 This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.